Saturday, August 10, 2013

DOUBLE J - FINAL! - Kazi mpya ya Jimmy Master!YULE muongozaji na mwigizaji Jimmy Mponda 'Jimmy Master' aliyetikisa
na mfululizo wa filamu za MISUKOSUKO sasa aja na filamu mpyainayoitwa Doble J Final  huku ujio huo ukiwa ni wa mwisho kutoka baada ya kutangulia  na Doble J sehemu ya kwanza na ya pili zilizotoka mwaka jana.

"Mwaka jana nilifanikiwa kukonga nyoyo za mashabiki wa filamu hususani wanaopagawa na filamu za mapigano na zilizojaa mambo ya  kipelelezi,"alisema Jimmy Master ambaye pia anajulikana kama J Plus.

Filamu hiyo ambayo Jimmy Master amemshirikisha mbabe mwingine katika filamu za mapigano Ibrahim Mbwana  'Bad Boy' na nyota wengine katika filamu kama Charles Magari, Hashim Kambi na Veronica Vyankero inatarajiwa kuwa sokoni mapema mwezi ujao.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO

There was an error in this gadget