Saturday, May 25, 2013

FLORA SHOW YAJA KUWASHIKA!!FLORA SHOW YAJA KUWASHIKA!!


WADAU wa  urembo nchini hususani Kanda ya Ziwa Victoria
wanatarajiwa kuneemeka kufuatia kuonekana kwa kazi zao kupitia kipindi
kipya kwenye luninga ya Star TV .

Mwanadada Flora Lawo  ameamua kumulika sanaa hiyo
kwa kuanzisha kipindi kitakacho itwa Flora Show katika kukuza
sanaa ya Urembo .

"Kuna mambo mengi ya kukuza urembo kama moja wapo ya
ajira hivyo hii itakuwa fursa tosha kwa namna moja ama
nyingine kwa wadau wa mambo ya Urembo na Utamaduni,'alisema
Flora.

Alisema kipindi hicho kitaanza kurindima rasmi    May  29  kupitia
luninga hiyo ya  Star TV, ambapo uzinduzi wa kipindi hicho utazinduliwa pia
Mwanza Hotel jijini humo katika siku hiyo ya May 29.

Wadau mbali mbali  kutoka makampuni mbali mbali wanakaribishwa
kuudhulia uzinduzi wa kipindi hicho, kwani kufika kwao  katika mchakato huo
kutaonesha kutoa sapoti katika kuutambua Urembo na Utanashati.

Pia kwa mujibu wa Emmanuel Shayo ambaye ni muhusika katika upande wa
Production amesema kuwa kipindi hicho kitakuwa bomba kutokana na hali
ya yeye kuwa ni mwenye uzoefu mkubwa katika masuala ya Production.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO

There was an error in this gadget