Friday, August 16, 2013

LISA: Kitabu cha hadithi katika michoro...LISA... ni Hadithi katika michoro iliyochorwa na SHAURI KATI (Shaka) Hadithi hii ilikuwa inatoka katika gazeti la IJUMAA na haikuweza kumalizika (Kufika Mwisho) sasa itapatikana katika kitabu kimoja kuanzia mwanzo mpaka mwisho kabisa wa kisa hicho ambacho asilimia 75 ni matukio ya kweli. 

Ili kujua Shaka alimtazamaje Dorice (Mkewe) baada ya kujua ya kuwa amekatwa mkono na mguu? Atataka kujua nini kuhusu mtoto aliyezaliwa Dorice? Mona naye ataishia wapi kwa unyama aliomfanyia Dorice (Wifi)?. Mama mwenye nyumba (Lisa) ataliacha SEKESEKE liishie hewani au ataendelea kukomaa na Mona na Shaka mpaka kieleweke? 

Majibu ya maswali yote haya utayapata ndani ya kitabu hiki cha LISA kitakachopatikana mitaani kuanzia tarehe 29 -08-2013 kwa bei ya shilingi 5,000/= tu. Hakikisha hukosi nakala yako.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kitabu hiki na kwa wanunuzi wa jumla wasiliana na : +255 715 492 199

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO